SERIKALI KUONGEZA VITUO VYA AFYA YA AKILI NCHINI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma SERIKALI imesema itaendela kuongeza vituo vya huduma ya afya ya akili nchini ili kuboresha utoaji wa huduma hiyo kwa lengo la kukabiliana na afya ya akili.Mratibu wa Hospitali za afya ya akili Tanzania Oresmos Mndeme amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua huduma ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu afya ya akili.